KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, December 11, 2010

Hasira za China zabubujika kuhusu NobelPicha ya mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel Liu Xiaobo iliyochukuliwa mwezi Machi mwaka 2005, mjini Guangzhou, kusini mwa China.
Umoja wa mataifa umesema kuwa maafisa nchini Uchina wamewakamata na kuwazuilia wanaharakati wasiopungua ishirini kabla ya kuandaliwa kwa sherehe za kutolewa kwa tuzo ya amani ya Nobel mjini Oslo leo Ijumaa.

Tuzo ya mwaka huu ilitolewa kwa mpinzani wa serikali ya uchini Liu Xiaobo anayehudumia kifungo cha miaka kumi gerezani kwa kuchochea maasi dhidi ya serikali.Picha za Liu Xiabo kwenye magazeti ya Uchina.
Kiti chake katika hafla hiyo ya Nobel kitabaki wazi.

China kadhalika imetoa amri ya kuzuiliwa nyumbani kwa wakosoaji wengi zaidi wa serikali na kuzuia vyombo vya habari vya kimataifa ikiwemo BBC.

Takriban thuluthi moja ya mataifa yaliyoalikwa kuhudhuria sherehe hizo yamesema yatasusia baada ya uchina kuonya kuwa ingelipiza kisasa kwa wale watakaohudhuria.

Uchina imesema kuwa kamati ya Nobel ilimchagua mhalifu kuhudumia maslahi ya mataifa kadhaa ya magharibi

No comments:

Post a Comment