KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, December 14, 2010

Congress yaidhinisha mkataba wa START


Bunge la Congress nchini Marekani limeidhinisha mkataba wa kupunguza umiliki wa silaha za Kinuklya kati ya marekani na Urusi, uamuzi ambao umetajwa na rais Barrack Obama kuwa muhimu zaidi wa aina yake katika kipindi cha takriban miaka ishirini.

Kura ya mwisho ilifanyika katika bunge la Senate, ambapo wabunge wa chama cha Republican walishawishiwa na wenzao wa Democrat kuunga mkono mkataba huo.


Mkataba wa START unalenga kupunguza zana za nuklya duniani.

Hatua hiyo ilijumuisha uungwaji mkono kutoka kwa mwanasiasa yeyote ambaye aliwahi kuhudumu kama waziri wa mashauri ya nchi za kigeni kutoka vyama vyote viwili. Mkataba huo unaofahamika kama, START, unapunguza zana za kivita zinazomilikiwa na mataifa yote mawili kwa kiasi cha thuluthi moja pamoja na kuondoa mabomu pamoja na nyambizi zenye zana za kinuklya.

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Urusi, Sergei Lavrov, ametaja kura hiyo kama sehemu muhimu ya mapatano ambayo tayari yametiwa saini na marais wote wawili mapema mwaka huu.

No comments:

Post a Comment