KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, December 14, 2010

Chenge anusurika kifungo, alipa faini

MBUNGE wa Bariadi Mashariki, Andrew Chenge amenusurika kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kufanikiwa kulipa faini ya shilingi laki saba baada ya Mahakama kumtia hatiani.

Hukumu hiyo ilitolewa jana katika mahakama ya Wilaya ya Kinondoni baada ya mbunge huyo kupatikanda na hatia ya makosa matatu na kila moja alitakiwa atumikie kifungo cha mwaka mmoja kila kosa.

Hukumu hiyo ilisomwa mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Kwey Lusema baada ya kupatikana na makosa matatu ya kusababisha vifo vya watu wawili, kuendesha gari kizembe ikiwemo na kuendesha gari bila kuwa na bima.

Chenge alisababisha vifo vya Victoria John na Beatrice Costatin baada ya gari alilokuwa akiliendesha kuigonga pikipiki ya miguu mitatu (Bajaj) ambayo marehemu hao walikuwa wamepanda.

Hivyo Hakimu Kwey alimtaka mshitakwia huyo kutumikia kifungo cha miaka mitatu ambapo kila kosa atatumikia kifungo cha mwaka mmoja au kulipa faini ya shilingi laki saba papohapo.

Hakimu alisema kama mshtiakiwa ataamua kulipa faini basi atalipa kama ifuatavyo “Katika shtaka la kwanza na pili atalazimika kulipa jumla ya faini ya shilingi laki tano, 500,000/= na katika shtaka la tatu ambalo ni la kuendesha gari wakati bima yake imemalizika muda wake atalipa faini ya sh laki moja100,000/= na sh 100,000/= kama faini ya uhalibifu wa mali, hivyo jumla ya fidia anayotakiwa kulipa kuwa ni sh laki saba 700,000/=.alimalizia hakimu

Vifijo na vigelegele vilitawala kwa ndugu na jamaa wa mbunge huyo na kukubali kulipa faini kumnusuru na kifungo hicho na kuitana pembezoni huku michango hiyo ikikusanywa na mke wa mshitakiwa na alionekana kuwa na furaha tele usoni mwake na kufanikiwa kuchangishana pesa na hatimaye waliwasilisha pesa hizo na kuondoka na ndugu yao huyo.









Hivyo kesi hiyo iliyodumu kwa muda mrefu jana ilifikia tamati baada ya kulipa faini hiyo hivyo kumfanya awe huru.

Hukumu hiyo ilionekana kuvutia watu wengi na kusababisha kuwa na umati wa watu mahakamani hapo kushuhudia hukumu ya mbunge huyo ambapo kila mmoja aliichukulia hukumu hiyo kwa mtazamo tofauti

No comments:

Post a Comment