KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, December 14, 2010

Boko Haram washambulia raia na polisi

Watu wanaoshukiwa kuwa Waisilam wenye itikadi kali wameuwa watu wasiopungua watano, wakiwemo maafisa watatu wa polisi, katika mashambulio kaskazini mwa Nigeria, kwa mujibu wa polisi.


Maiduguri


Kamanda wa polisi wa jimbo la Borno amesema watu 92 wamekamatwa tangu mashambulio hayo kufanyika siku ya Jumatano katika jiji la magharibi la Maiduguri.

Watu waliofanya mashambulio hayo wanashukiwa kuwa wafuasi wa kundi la Boko Haram

Kamanda wa polisi wa Borno

Mapigano kati ya kundi hilo na polisi yamesababisha vifo vya mamia ya watu tangu mwaka jana.

Kundi la Boko Haram lilidai kuhusika na mashambulio ya mabomu ya siku ya kuamkia Krismasi katika jiji la Jos ambayo yalisababisha vifo vya watu wapatao 80.

Bomu

Mkuu wa polisi kamishna Mohamed Abubakar Jinjiri ameiambia BBC Idhaa ya Kihausa kuwa watu watano wameuawa katika mashambulio hayo. Amesema miongoni mwa waliokamatwa ni mtu anayeshukiwa kuwa mdhamini wa Boko Haram, ambaye alikuwa na vifaa vya kutengenezea bomu nyumbani kwake.

Wakati huohuo msemaji wa jeshi, Luteni Abubakar Abdullahi ameliambia shirika la habari la AFP kuwa watu wanane wameuawa katika mashambulio mengine

No comments:

Post a Comment