KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, December 14, 2010

Bingwa wa Olimpiki, Wanjiru, mahakamani

Bingwa wa Olimpiki Samuel Wanjiru amefikishwa mahakamani nchini Kenya na kufunguliwa mashtaka ya kutishia kumuua mkewe Teresia.


Bingwa wa Olimpiki, Samuel Wanjiru


Wanjiru ambaye pia ni mshindi mara mbili wa mbio za masafa marefu ya Boston alishtakiwa na kuwa na silaha kinyume cha sheria mbali na kutishia kumuua msaidizi wake wa nyumbani Bi. Nancy Njoki na pia kumjeruhi mlinzi wake William Masinde.

Wanjiru alikana mashtaka hayo mbele ya hakimu mkuu mkaazi wa nyahururu na kuachiliwa kwa dhamana ya shilling laki tatu za kenya na mdhamini na kiasi kama hicho.

Mahakama hiyo ilifahamishwa kuwa wanjiru alifanya uhalifu huo usiku hapo jana katika mtaa wa Muthaiga mjini Nyahururu.

Maafisa wa polisi walimkamata mwanariadha huyo jana usiku na kumzuilia hadi baada ya kesi hiyo iliposikilizwa hii leo.

Hakimu mkuu mkaazi wa nyahururu Bi Alice Mong'are amesema kesi hiyo itasikilizwa tarehe tisa mwezi ujao.

No comments:

Post a Comment