KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, December 10, 2010

Biashara ya wahamiaji yapigwa vita




Wahamiaji wengi kutoka Afrika ni sehemu tu ya idadi inayoongezeka ya wahamiaji wanaotumia njia kupitia Misri wakijaribu kuvuka na kuingia Israili kinyume cha Sheria.

Inadhaniwa kuwa Watu wanaovusha wahamiaji, ni kutoka makabila ya wa Bedouin wakiwavusha jangwa la Sinai. Lakini kwa mujibu wa habari zilizojitokeza hivi karibuni kutoka kwa wahamiaji wenyewe, wavusha wahamiaji wamepandisha kiwango cha ada ya malipo waliokuwa wakitoza kuanzia dola elfu mbili hadi elfu nane na hata elfu kumi na tano.


Endapo utashindwa kulipa au ukikataa,basi utawekwa ndani ya container kwa kipindi kirefu hadi miezi sita katika mazingira mabovu na magumu.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi linasema kuwa limehakikishiwa na serikali ya Misri kuwa limeanzisha juhudi za masaa ishirini na manne kuwatafuta na kuwaokoa wahamiaji wa aina hiyo.

Njia inayopitia Sinai imezidi kutumiwa na watu wanaohamisha wahamiaji wakati Mataifa ya Afrika ya kaskazini yameweka mikakati ya kuzuia shughuli kama hiyo ya kuhamisha watu kuelekea Ulaya.

Mara kwa mara Vikosi vya usalama vya Misri hupambana na makundi yanayohamisha watu katika ardhi yao, wakati Israili nayo hivi karibuni ilianza ujenzi wa ukuta mkubwa kwenye mpaka wake wa Jangwani baina yake na Misri kujaribu kuzuwia biashara ya binaadamu

No comments:

Post a Comment