KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, December 14, 2010

Bashir atakubali matokeo ya Sudan Kusini

Rais Bashir wa Sudan

Rais wa Sudan Omar al Bashir amesema atakubali uamuzi wowote ambao Sudan Kusini itaufanya katika kura ya maoni ya uhuru wa eneo hilo mwezi wa Januari mwakani.

Rais Bashir amesema Sudan Kaskazini itatoa msaada wowote utakaohitajika kwa Kusini, kama wataaamua kujitenga au la.

Bashir alikuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika eneo la Al-Jazira katikati mwa Sudan.

Alisema serikali ya Sudan itawasaidia watu wa Kusini kuijenga nchi yao, kwa vile inataka taifa hilo liweze kujiendesha bila matatizo.

Rais Bashir mapemwa mwezi wa Desemba alisema sehemu ya kaskazini mwa Sudan, ambapo kuna Waislamu wengi, itaimarisha sheria za Kiislamu ama sharia, baada ya kura ya maoni.

No comments:

Post a Comment