KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, December 15, 2010

Assange aachiwa kwa dhamana



Muanzislishi wa tovuti ya WikiLeaks Julian Assange ameachiliwa kutoka jela. Jaji wa mahakama moja ya Uingereza alimuachilia Assange kwa dhamana baada ya kutupilia mbali rufaa ya Sweden, iliyopinga uamuzi wa awali wa kumuachia huru kwa dhamana. Assange mwenye umri wa miaka 39 hata hivyo bado anakabiliwa na changamoto nyingine, ya kurejeshwa nchini Sweden, ambako waendesha mashtaka wanataka kumhoji zaidi kuhusiana na madai ya ubakaji. Raia huyo wa Australia alisema atahakikisha analisafisha jina lake kutokana na madai hayo ya ubakaji, na pia ataendelea na majukumu yake katika tovuti yake ya WikiLeaks. Kwa sasa Assange ataishi nchini Uingereza hadi pale kesi yake itakaposikizwa tena mwaka ujaao. Yeye pamoja na wanasheria wake wameshikilia kuwa harakati za kumrejesha Sweden ni za kisiasa. Wanaamini kuwa Marekani inataka kumshtaki kwa kosa la ujaasusi. Marekani imeghadhabishwa na hatua ya WikiLeaks kuzitoa kwa umma nyaraka zake za siri

No comments:

Post a Comment