KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, December 14, 2010

Afrika kujaribu tena kumshawishi Gbagbo

Viongozi watatu wa mataifa ya Afrika Magharibi, watarejea tena nchini Ivory Coast siku ya Jumatatu kwa ajili ya majadiliano zaidi ya kumaliza mzozo wa kisiasa uliodumu kwa miezi kadhaa.


Waandamanaji wanaomuunga mkono Alassane Ouattara


Tangazo hilo limekuja siku moja baada ya viongozi hao kushindwa kumshawishi Bw Laurent Gbagbo kuachia madaraka.

Mwenyekiti wa jumuiya ya kiuchumi ya Afrika Magharibi, Ecowas, ambaye pia ni rais wa Nigeria Goodluck Jonathan amesema mazungumzo bado yanaendelea.

Mshindi halali

Ecowas ina matumaini kuwa Bw Gbagbo atakubali kuachia ngazi na kumpisha Alassane Ouattara, ambaye anaaminika kuwa ndio mshindi halali wa uchaguzi.

Jumuiya hiyo imetishia kutumia nguvu iwapo atagoma kuondoka madarakani

Mwenyekiti wa Ecowas, Goodluck Jonathan


Kituo cha televisheni cha serikali kimetangaza kuwa mamilioni kadhaa ya wafanyakazi kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika wanaofanya shughuli zao nchini Ivory Coast, watakuwa hatarini iwapo nguvu za kijeshi zitatumika.

"Watarejea tena Januari 3, na watakaporudi, matokeo yake ndio yataamua hatua itakayochukuliwa," amesema Rais Jonathan.

"Panapotokea mzozo, panapokuwa na kutokuelewana, ni mazungumzo ndio yatatatua". amesema rais huyo wa Nigeria.

No comments:

Post a Comment