KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, September 7, 2010

Tendwa atupilia mbali pingamizi la Chadema


MSAJILI wa Vyama vya siasa nchini, John Tendwa alishindwa kutoa majibu didi ya pingamizi lililowasilishwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeo [CHADEMA] kwa kuwa si la msingi.
Tendwa alitoa majibu hayo jana ofisini kwake mbvele ya waandishi wa habari na kusema ametupilia mbali pingamizi hilo kwa kuwa ameona halina msingi na angeweza kutoa majibu hayo yangeweza kuhatarisha amani ya nchi.

Alisema pingamizi hilo limeshindwa kuthibitishwa na tume hiyo hivyo majibu dhdi ya pingamizi hilo hayataweza kupoatikana.

Alisema pingamizi hilo limepokelewa kwa aina tofauti tofauti na wanaweza wakahatarisha amani ya nchi hivyo tume imeamua kutupilia mbali kwa kuwa hawakuweza kuthibitisha.
“Unajua tuhuma hizo zinalazimika ziepukwe ili kuondoa migongano isiyo ya lazima” Tendwa

Septemba Mosi mwaka huu, Chadema iliwasilisha pingamizi lao dhidi ya mgombea wa urais wa chama cha Mapinduzi kwa kudai kutumia nafasi yake ya urais vibaya na kushawishi wananchi kumpigia kura kwa kutoa ahadi za kuongeza mishahara katika kampeni na kutoa ahadi nyingi katka kampenei hizo kwa kudai alikiuka sheria za uchaguzi nchini.

Pingamizi hilo liliwasilishwa na Kaimu Katibu Mkuu wa chadma hicho, John Mnyika na Msajili huyo alijibu kutoa uamuzi dhdi ya pingamizi hilo baada ya siku tano ambayo ni jana na majibu hayo hayakuweza kutolewa kwa sababu zilizoelezwa hapo juu.

No comments:

Post a Comment