KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Tuesday, September 7, 2010

Saadane ajiuzulu


Shirikisho la soka la Algeria limethibitisha kwamba kocha wa timu ya taifa Saadane amejiuzulu, mara tu baada ya timu yake ya Desert Foxes kutoka sare ya 1-1 na Taifa Stars ya Tanzania.


Desert Foxes hawakuamini sare ya 1-1
Ilikuwa ni mechi ya kufuzu kushirikishwa katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2012, iliyochezewa mjini Algiers.

Shirikisho la soka Algeria lilielezea kwamba kocha huyo aliandika barua ya kutaka kujiuzulu kufuatia matokeo ya kuvunja moyo, na shirikisho kuikubali hatua hiyo.

Saadane alianza kuifundisha timu hiyo miaka mitatu iliyopita, na akaweza kuiongoza timu hadi mashindano yake ya kwanza ya Kombe la Dunia yaliyofanyika nchini Afrika Kusini.

Algeria iliweza kufuzu kufika huko baada ya kipindi cha miaka 24.

Lakini timu ilirudi nyumbani mapema, baada ya kupata pointi moja tu, kufuatia mechi tatu katika kiwango cha makundi.

Shirikisho la soka la Algeria hata hivyo halikutangaza moja kwa moja ni nani atayachukua madaraka ya kocha huyo wa 'Mbweha wa Jangwani".

Saadane, mwenye umri wa miaka 64, awali alifikiria kujiuzulu baada ya timu yake kuondolewa mapema katika mashindano ya Afrika Kusini pasipo kufunga bao, lakini akaamua kuendelea.

Timu hiyo ilishikilia mkia katika kundi C, baada ya kushindwa na Slovenia, Marekani na kutofungana na England.

The federation did not immediately say who would replace Saadane as coach of the Desert Foxes.

Kwa bahati mbaya, licha ya kufika nusu fainali katika mashindano ya Kombe la Mataifa nchini Angola mwezi Januari, Algeria imeanza vibaya kampeni yake ya mwaka 2012, kwa sare hiyo ya 1-1 dhidi ya Taifa Stars mjini Algiers.

Wageni Taifa Stars ndio waliokuwa wa kwanza kuongoza katika mechi hiyo ya kundi D, kupitia mkwaju wa Abdi Kassim, kutoka yadi 30, katika dakika ya 33

No comments:

Post a Comment