KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Tuesday, September 7, 2010

Rooney kwenda Uswiss licha ya kashfa


Mshambuliaji Wayne Rooney amesafiri na kikosi cha England kwa ajili ya pambano la kufuzu kucheza fainali za Euro dhidi ya Switzerland licha ya tuhuma zinazohusiana na maisha yake binafsi.

Chama cha Soka cha England kimethibitisha kusafiri kwa Rooner. Mchezaji huyo amesafiri na kikosi cha England kitakachocheza siku ya Jumanne katika kundi lao la C.

Hata hivyo, kocha wa England Fabio Capello atalazimika kuamua iwapo Rooney yupo makini kimawazo kucheza mechi hiyo. Habari zilizotolewa na gazeti la News of the World pamoja na Sunday Mirror, zimefichua taarifa hizo na magazeti yote ya udaku ya Uingereza yalisheheni habari za kashfa ya Rooney kwenda nje ya ndoa.

Rooney alifanya kazi nzuri wakati England ilipowalaza Bulgaria mabao 4-0 katika uwanja wa Wembley siku ya Ijumaa, baada ya kutocheza vizuri wakati wa mashindano ya Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment