KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, September 6, 2010

Rais Kagame kuapishwa kwa muhula wa piliRais Paul Kagame

Baadhi ya marais wa nchi za kiafrika wamewasili nchini Rwanda kwa sherehe za kumuapisha upya rais wa nchi hiyo Paul Kagame.

Kagame anaapishwa kuhudumu kwa muhula wa pili ofisini baada ya kushinda uchaguzi uliofanyika mwezi wa saba.

Aidha Kagame alichaguliwa tena kwa asilimia tisini na tatu ya kura zilizopigwa mwezi jana ingawa anaapishwa huku nchi yake ikikabiliwa na shutuma za jeshi kuhusika na mauaji ya halaiki ya watu katika nchi jirani ya Congo.

Hata hivyo baadhi ya viongozi wa upinzani walizuiwa kushiriki kwenye uchaguzi huo wengi wakiseama ni hali ya mbaya ya kisiasa iliyochochea kususia kwao. wamedai kuwa rais Kagama anawakandamiza kisiasa

No comments:

Post a Comment