KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, September 6, 2010

Marubani wachunguzwa Uchina


Marubani wachunguzwa Uchina

Marubani wa Henan walitoa maelezo ya uwongo kuhusiana na ujuzi wao
Uchina imeanza kuwachunguza marubani wake wote wanaohusika katika safari za ndege za abiria, kufuatia madai kwamba zaidi ya marubani mia mbili walitumia vyeti vyenye maelezo ya uwongo, kuhusiana na ujuzi na maarifa yao ya urubani.

Idara ya safari za ndege iligundua kwamba zaidi ya marubani mia moja waliotoa maelezo ya uwongo walikuwa ni wafanyikazi wa shirika la ndege la Shenzhen, kampuni kuu iliyosimamia shirika la ndege la Henan, ambalo ndege yake ilianguka mwezi uliopita, na kusababisha vifo vya watu arubaini na wawili.

Zaidi ya watu 54 walinusurika baada ya ndege hiyo kukosea njia.

Kati ya mwaka 2008 hadi 2009, inaelekea maelezo kuhusiana na historia ya kikazi ya zaidi ya marubani 200 wanaohusika na ndege za abiria ni ya uwongo, na wengi wakitia chumvi juu ya maarifa yao.

Ripoti hiyo inaelezea kwamba kati ya marubani wanaohusika ni wale waliokuwa wakiendesha ndege za kijeshi, na baadaye kuanza kuendesha ndege za abiria.

Baada ya kugunduliwa, marubani hao wanakatazwa kufanya kazi, hadi watakapokaguliwa na kutahiniwa tena.

Sekta ya safari za ndege nchini Uchina imekuwa ikiimarika kwa kasi mno, na kila mwaka mamia ya marubani uhitajika.

No comments:

Post a Comment