KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, September 7, 2010

Kocha Ghana atakiwa kusaini mkatabaMilovan Rajevac

Kocha wa timu ya taifa ya Ghana, Black Stars Milovan Rajevac amepewa muda wa siku saba kusaini mkataba mpya aliopewa na Chama cha Soka cah nchi hiyo (GFA)

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 56 amepewa mkataba mpya wa miaka minne, lakini bado hajasaini kuitokana na mzozo wa mkataba na meneja wake.

Mwenyekiti wa GFA Kwesi Nyantakyi amesema Rajevac anatakiwa kusaini haraka.

Nyantakyi ameiambia BBC kwamba iwapo kocha huyo atashindwa kutatua suala hilo haraka, basi watatafuta kocha mwengine.

Rajevac aliifikisha timu hiyo ya taifa ya Ghana ikiwa na vijana wadogo hadi katika fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Angola mwezi wa Februari na pia hadi hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia miezi michache iliyopita nchini Afrika Kusini, hali iliyosababisha mashabiki na wachezaji wa nchi hiyo kutaka mkataba wake urefushwe.

Nyantakyi amesema anatumaini suala hilo litatatuliwa haraka iwezekanavyo.

Mwenyekiti huyo wa Chama cha Soka cha Ghana amebainisha kwamba Rajevac anataka kubakia nchini humo licha ya kupokea vishawishi vinono kutoka nje.

No comments:

Post a Comment