KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Tuesday, September 7, 2010

Dirk Kuyt aumia kutocheza wiki nne
Dirk Kuyt

Mshambuliaji wa Liverpool Dirk Kuyt hataonekana uwanjani kwa wiki nne baada ya kuumia bega wakati akiichezea timu yake ya taifa ya Uholanzi.

Kuyt mwenye umri wa miaka 30 aliumia mazoezini akijiandaa kwa pambano la kufuzu kwa makundi kuwania ubingwa wa Ulaya watakapocheza na Finland siku ya Jumanne na amerejea Liverpool kwa uchunguzi zaidi.

Daktari wa Liverpool Peter Brukner amethibitisha, mchezaji huyo hatacheza soka kwa wiki nne.

Kuyt alimuia bega baada ya kuanguka vibaya katika uwanja wa ADO Den Hague.

Mshambuliaji huyo alifunga bao kwa mkwaju wa penalti wakati Uholanzi ilipoifunga mabao 5-0 San Marino katika mchezo wa ufunguzi wa kundi la E siku ya Ijumaa.

Pia alipachika bao wakati Liverpool ilipoifunga Trabzonspor mabao 2-1 katika kombe la Uefa.

Kuyt amekuwa akihusishwa kujiunga na klabu ya Inter Milan chini ya meneja wa zamani wa Liverpool Rafael Benitez, lakini baada ya mechi na Trabzonspor, mshambuliaji huyo alithibitisha ataendelea kuichezea Liverpool.

Kwa kuwa nje kwa wiki nne, Kuyt atakosa mechi dhidi ya Birmingham, Steaua Bucharest, Manchester United, Northampton, Sunderland na mechi ya kombe la Europa dhidi ya klabu ya Utrecht

No comments:

Post a Comment