KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, September 6, 2010

Ajali ya boti nchini DRC yasababisha maafa



Boti ikiwabeba abiria nchini Congo

Watu wengi wanahofiwa kufa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo baada ya boti mbili kupinduka katika matukio tofauti. Mojawapo ya boti hizo iliripotiwa kubeba abiria kufikia mia tatu.

Kulingana na ripoti, abiria waliruka kwenye maji wakati engine ya boti hiyo iliposhika moto wakati ikipita kijiji cha Mbendayi kwenye mto wa Kasai karibu na mpaka na Angola.

Kwa mujibu wa waziri wa habari wa Congo boti hiyo ilikuwa ikisafirisha mafuta na haikutakiwa kubeba abiria yeyote.

Taarifa kutoka katika jimbo la kaskazini magharibi la Equateur zinaarifu kuwa zaidi ya watu sabini wanaaminika kufa maji baada ya boti yao kugonga jabali mnamo jumamosi.

No comments:

Post a Comment