KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, September 6, 2010

Aangua kilio baada ya kutapeliwa- Kar iakoo



KATIKA pilikapilika za maandalizi ya sikuuu ya Idd, matapeli wengi kutoka kona mbalimbali za jiji la Dar es Salaam wamemwagika kwa wingi katika maeneo ya Kariakoo ili na wao kujitafutia riziki kwa njia ya udanganyifu.
MWanamke mmoja, Fatuma jana, alijikuta akiwa katika wakati mgumu baada ya kutapeliwa pesa kiasi cha shilingi elfu 50 na mtu ambaye alijitambulisha ni muhusika katika moja ya madukani yaliyopo Kariakoo.

Mwanamke huyo alitapeliwa na mtu huyo kwa kumuamini ni muhusika dukani hapo na kumkabidhi pesa hiyo ili akamletee pea mbili za viatu za watoto wake katika moja ya duka lingine wanayoshirikiana nayo kibiashara.

Alidai mara baada ya kufika nje ya duka hilo, alichagua viatu alivyokuwa ameshika mujuzaji huyo nje ya duka hilo,ila hakupatika namba anayoihitaji kwa watoto wake hao, hivyo kijana huyo alimtaka mwanamke huyo amkabidhi pesa hizo ili akamletee pea hizo duka linguine ambapo alidai alimueleza kuwa ni ya tajiri mmoja.

Hivyo mwanamke huyo, bila kutambua kama kijana huyo alikuwa akiendesha shughuli hizo kitapeli, aliweza kumkabidhi pesa hizo bila kuwaatarifu wengine dukani humo.

Hivyo aliweza kustaajabu dakika zililizidi kusogea na ndipo alipowauliza wauzaji wa dukanai humo kuwa hilo duka linguine liko umbali gani, na wauzaji hao wakamueleza huyo kijana alikuwa hahusiki dukani humo.

Ndipo mwanamke huyo alianza kilio asichokitarajia huku akishangaliwa na wengi waliptao njia hiyo na kuwalilia wenye duka hilo.

Kipindid hiki cha sikukuuu kumekuwa na wizi haa maeneo ya Kariakoo

No comments:

Post a Comment