KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, August 12, 2010

Zardari ajionea mafurikoRais wa Pakistan, Asif Ali Zardari, ameutembelea mkoa wa Sindh, ili kujionea mwenyewe uharibifu uliosababishwa na mafuriko ambao haujawahi kuonekana katika eneo hilo.
Asif Ali Zardari

Rais wa Pakistan alilaumiwa kwa kukataa kufupisha ziara

Ziara yake Sukkur ilikuwa ya kwanza, tangu kurudi nchini Pakistan kutoka Ulaya, siku mbili zilizopita.

Bw Zardari amekuwa akilaumiwa vikali nchini humo kwa kukataa kusitisha ziara yake ng'ambo, licha ya uharibifu mkubwa uliofanywa na mafuriko hayo.

Waziri wa masuala ya chakula nchini Pakistan, Nazar Muhammad Gondal, amesema baadhi ya maghala ya nafaka nchini humo huenda yakawa yameahribiwa na mafuriko.

Alisema mavuno mengi ya msimu huu pia huenda yakawa yameharibiwa na mvua, na ameitaka jamii ya kimataifa kutuma misaada.

No comments:

Post a Comment