KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, August 16, 2010

Wataalam wa Ufaransa kuchunguza kifo cha Habyarimana.


Serikali ya Ufaransa itawatuma wataalam nchini Rwanda kuchunguza kifo cha aliyekuwa rais wa nchi hiyo Juvenal Habyarimana.

Miongoni mwa wataalam hao ni jaji mpya wa Ufaransa Marc Trevedich aliyechukua nafasi ya Jean Luis Brugiere.

Ubalozi wa Ufaransa nchini Rwanda umetangaza kuwa jaji huyo anatarajiwa kuwasili Rwanda mwanzoni mwa mwezi Septemba mwaka huu. Pamoja na mambo mengine wataalam hao wanaomba kukutana ana kwa ana na maafisa wanaotuhumiwa.

Msemaji wa jeshi la Rwanda Luteni Kanali Jean Rutalemala anasema, "La muhimu ni kubainisha ukweli watakapokutana na wahusika katika kesi hiyo lakini pia na mashahidi wengine na kuzuru eneo la tukio. Kingine wakituomba tutawasaidia kwa kuzingatia uwezo tulionao."

Tangazo la mpango huo limekuja baada ya Rwanda na Ufaransa kurejesha uhusiano wa kidiplomasia. Moja ya sababu kubwa zilizosababisha kuvunjika kwa uhusiano huo ni vibali vilivyotolewa na jaji wa zamani Jean Luis Bruguire vikitka wakamatwe maafisa kadhaa wa jeshi la Rwanda kwa kuhusishwa na utunguaji wa ndege ya Rais Habyarimana.

Balozi wa Ufaransa nchini Rwanda Laurent Contini ameiambia BBC kuwa kujiuzulu kwa jaji Bruguire ni hatua muhimu katika uhusiano wa nchi hizi mbili.

Mbali na suala hilo, Balozi huyo wa Ufaransa amesema nchi yake imenuia kufufua uhusiano wa kijeshi na Rwanda.

Ufaransa ilikuwa mshirika mkubwa kijeshi wa serikali ya hayati Habyarimana, jambo lililosababisha mifarakano ya muda mrefu na serikali ya Rwanda ya RPF chini ya Rais wa sasa Paul Kagame.


No comments:

Post a Comment