KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, August 10, 2010

Wafuasi wa Kagame waanza Sherehe Rwanda


Ilikuwa ni matokeo ya kura zilizopigwa na Wanyarwanda wanaoishi nje ya nchi.

Matokeo hayo yaliyoonyeshwa kwenye skrini kubwa humo yalionyesha Bwana Kagame na ushindi wa 96%. Kitaifa bado kura zinahesabiwa.

Japo Matokeo haya yalitarajiwa, Rais Kagame alitia bidii zaidi katika kampeini zake. Wengi wamehoji kuwa huenda alichangamkia kampeini hivyo ili kuweka taswira kwa jamii ya kimataifa kuwa ushindi wake ulitokana na kazi ngumu ya kidemokrasia.

Kagame sasa anakabiliwa na changa moto kubwa katika uongozi wake wa muhula huu wa pili, kujisafishia jina lake na labda kulegeza kamba kidogo na kurejesha demokrasia. Amelaumiwa pakubwa na jamii ya kimataifa kwa namna alivyokuwa na uongozi wa kibabe katika muhula wake wa kwanza kama rais. Pia huenda akashughulikia kumteua kiongozi atakayempokeza baada ya miaka saba.

Upinzani nao umekuwa ukimshutumu Kagame kwa kuwanyima haki sawa ya kukampeini na hata baadhi yao kukosa kusajiliwa kama wagombea halali.

Tume ya uchaguzi inatarajiwa kutangaza matokeo rasmi punde tu itakapokamilisha kujumuisha.

No comments:

Post a Comment