KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, August 11, 2010

Uchaguzi wa Rwanda: wachunguzi wakosoa


Wachunguzi wa jumuiya ya madola walioko nchini Rwanda wamesema uchaguzi wa urais uliofanyika Jumatatu ulikosa sauti ya upinzani na hivyo kuwa na mtazamo kuwa hapakuwa na ushindani baada ya baadhi ya wapinzani kuzuiwa kugombea uchaguzi huo.

Rais Paul Kagame anatarajiwa kupata ushindi wa kishindo kwa zaidi ya asilimia tisini ya kura. Wakati bwana kagame akisifiwa kwa kumaliza mauaji ya kimbari na kuimarisha ukuaji wa uchumi, serikali yake imekosolewa kwa kuwabana wapinzani.

Baadhi ya wagombea wa Urais wa upinzani walinyimwa vibali vya kushiriki uchaguzi huo na wale waliosajiliwa walinyimwa uhuru wa kujifanyia kampeini

No comments:

Post a Comment