KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Sunday, August 29, 2010

Ravalomanana ahukumiwa kifungo








Rais wa Madagascar anayeishi uhamishoni, amepewa hukumu ya kifungo cha maisha jela, na kazi ngumu kwa kutoa amri ya mauaji ya wafuasi wa upinzani.
Marc Ravalomanana

Jela maisha na kazi ngumu

Marc Ravalomanana alihukumiwa bila ya yeye kuwepo mahakamani, kufuatia mauaji yaliyotokea mwezi Februari 2009, ya watu wasiopungua 30 na walinzi wake.

Bw. ravalomanana amekuwa akiishi nchini Arika Kusini tangu mezi machi mwaka 2009.

Watu waliouawa walikuwa wafuasi wa Andrey Rajoelina, ambaye hivi sasa ni rais.
Ravalomanana

Ravalomanana amehukumiwa bila kuwepo mahakamani

Bw. ravalomanana alishitakiwa kwa makosa ya mauaji na kuhusika katika mauaji, pamoja na washitakiwa wengine 18, wengine pia wakiwa wanaishi uhamishoni.

Wakili mtetezi wa rais wa zamani, waliondoka mahakamani muda mfupi baada ya kesi kuanza kusikilizwa, wakisema mahakama hiyo inatumiwa na utawala wa Bw. Rajoelina.
Rajoelina

Rais Andry Rajoelina

"Lengo ni kumhukumu ili asiweze kurejea Madagascar na kushiriki katika uchaguzi siku zijazo," wakili Hanitra Razafimanantsoa ameliambia shirika la habari la AFP.

Madagascar imekuwa katika mtikisiko wa kisiasa katika kipindi cha meizi 19 iliyopita.

Hii ni hukumu ya tatu kutolewa kwa Bw. Ravalomanana tangu alipoondoka nchini humo.

No comments:

Post a Comment