KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Monday, August 9, 2010

Rais wa Zamani wa Uganda Afariki Dunia

Aliyekuwa rais wa sita wa Uganda Godfrey Lukongwa Binaisa amefariki dunia usingizini akiwa na umri wa miaka 90.
Rais wa zamani wa Uganda Godfrey Lukongwa Binaisa alifariki dunia usiku wa kuamkia ijumaa kwenye nyumba yake katika kitongoji cha Kizungu mjini Kampala.

Binaisa ambaye alikuwa ni rais wa sita wa Uganda, alifariki dunia akiwa usingizi.

"Tuna huzuni sana", alisema binti wa Binaisam Nakalema Binaisa huku akijifuta machozi yaliyokuwa yakitiririka kwenye macho yake.

"Alienda kulala huku akitabasamu lakini hakuweza kuamka asubuhi", alisema Bi Nakalema.

"Tulienda hospitali jumatatu na tuliambiwa kiwango cha sukari kwenye damu yake kipo chini, tulirudi nyumbani na alionekana yupo fiti, alimwita nesi wake ampime kiwango chake cha sukari kabla hajalala, lakini asubuhi hakuweza kuamka", alisema.

Binaisa alikuwa rais mwaka 1979 akichukua nafasi ya Yusuf Lule, aliyekuwa rais wa mpito kwa siku 68 baada ya kupinduliwa kwa rais Idi Amini.

Mwili wa Binaisa unatarajiwa kuzikwa jumatano.

No comments:

Post a Comment