KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Friday, August 13, 2010

MWanamke aiba mtoto Temeke


MWANAMKE mmoja asiye na hata chembe ya woga, jana aliibuka katika hospitali ya Wilaya ya Temeke na kuiba kichanga cha jinsia ya kike, chenye wiki moja, aliyekuwa amelazwa na mama yake hospitali hapo.
Taarifa iliyothibishwa na Kamanda wa Polisi, Mkoani Temeke, Bw. David Misime, ilisema kuwa, mtoto huyo mwenye umri usiozidi wiki moja aliibiwa kwa njia za ujanja kwa kurubuniwa na mwanamke huyo.

Alisema mwanamke huyo alimuhadaa shangazi wa mtoto kwa kumpa fedha akamnunulie supu kwa kutumia upenyo huo kwa kuwa alipomuuliza kama mzazi alikunywa supu alimjibu supu haikufika toka nyumbani, na alimpa pesa na kumuamuru atoke nje ya hospitali hiyo akanunue supu ya mama wa mtoto.


Alisema wakati shangazi huyo alipokwenda kununua supu hiyo, mwanamke huyo alisogea karibu zaidi na kitanda na kuzungumza na mama wa mtoto huyo mithili ya mtu anayemfahamu na kumsemesha kwa mazungumzo ya hapa na pale .

Alisema wakati shangazi huyo alipokwenda nje kununua supu hakufanikiwa kupata supu kwa sehemu aliyokwenda awali kwa kuwa alijibiwa hawana chenji alikuwa na noti ya shilingi elfu kumi na kurudi kumueleza mwanamke huyo aliyejifanya msamalia na kumueleza aende sehemu nyingine na yeye angebaki na mtoto wodini hapo ndipo alipopata fursa ya kuondoka na mtoto huyo.

Aliporudi hakumkuta dada huyo na kichanga hicho hakikikuwepo kitandani hapo na kutoa taarifa kuhusiana na atukio hilo.

Kamanda Misime amesema,Polisi wanaendelea kumtafuta mtuhumiwa huyo.

No comments:

Post a Comment