KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, August 12, 2010

Morocco kufunga misikiti 'isiyo salama'


Serikali ya Morocco imesema itafunga misikiti 1,256 inayoonekana kutokuwa salama ili kuzuia tukio jengine la kuporomoka kwa mnara wa msikiti mwezi Februari ulioua watu 41.

Waziri wa masuala ya dini alisema zaidi ya misikiti 500 itavunjwa na kujengwa upya.

Wizara hiyo imesema vyumba vya muda na mahema vitawekwa kwa ajili ya swala.

Mfalme Muhammed ameamuru misikiti yote nchini humo ikaguliwe upya baada ya mnara mkongwe wa msikiti uliodumu kwa miongo mingi huko Meknes ulipoporomoka wakati wa swala ya Ijumaa.

Ajali hiyo iliibua ukosoaji mkubwa kwa serikali kutoka kwa umma kutokana na kukosa kuhudumia misikiti hiyo.

Wizara inayoshughulika na masuala hayo ya dini ilisema baada ya kukagua misikiti 19,205 ya nchi hiyo miongoni mwa 48,000, iliamuliwa ifungwe kabisa kwa asilimia 6.5.

Imesema dola za kimarekani milioni 325 zimetengwa kwa ajili ya kuboresha misikiti hiyo, ikiwa ni pamoja na kuvunja na kujenga upya misikiti 513.

Msikiti huo huko Meknes, ambapo mji wake wa kihistoria uko katika orodha za kumbukumbu za kiasili za Umoja wa Mataifa, ni miongoni mwa majengo yanayojengwa upya.

No comments:

Post a Comment