KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, August 10, 2010

Mawaziri 4 wafutwa kazi Malawi

Rais wa malawi Bingu wa Mutharika amewafuta kazi mawaziri wake wanne wa muda mrefu katika mabadiliko yake ya kwanza ya baraza la mawaziri tangu alipochaguliwa tena mwaka jana. Mawairi hao wanne walikuwa katika wizara za serikali za mitaa, afya, uchukuzi na maendeleo ya jamii.
Waandishi wa BBC wanasema kuwa waziri wa serikali za mitaa Goodall Godwe ambaye awali alikuwa waziri wa fedha amekuwa muhimu katika kuimarisha mfumo wa fedha za umma.
Kumekuwa na tetesi kwenye vyombo vya habari vya ndani ya nchi hiyo kwamba mageuzi hayo huenda yanahusiana na kuongezeka kwa umaarufu wa kaka yake rais, Peter Mutharika katika siasa za nchi hiyo

No comments:

Post a Comment