KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, August 9, 2010

Mashindano ya Kutafuta Kifo


Mwanaume mmoja wa nchini Urusi, amefariki dunia baada ya mwili wake kubabuka wakati wa mashindano ya kukaa ndani ya chumba chenye joto la nyuzi joto 110.
Vladimir Ladyzhenskiy, mwanamieleka mwenye umri wa miaka 60 alifariki dunia jumamosi wakati wa akiwania ubingwa wa mashindano ya sauna kustahmili kukaa kwenye joto kali kwa muda mrefu.

Ladyzhenskiy alifariki kwenye joto la nyuzi joto 110 akiwa pembeni ya bingwa mtetezi Timo Kaukonen wa Finland zikiwa zimebakia dakika sita kuingia raundi ya mwisho.

Zaidi ya watu 1,000 walikusanyika kwenye mji wa kusini mwa Finland wa Heinola kuwaangalia watu 130 toka nchi 15 wakishindana kukaaa kwenye chumba chenye joto kali.

Video ya tukio hilo ilionyesha watoa huduma za kwanza wakiiziba steji kwa turubai na kuwamwagia maji ya baridi wanaume wawili ambao walizidiwa na joto kali.

Wanaume hao walikuwa wakitiririka damu ambazo inaaminika zilikuwa zikitoka kwenye majeraha ya kuungua waliyopata.

Mashindano hayo ambayo yalianza mwaka 1999 yamepigwa marufuku na hayatafanyika tena.

No comments:

Post a Comment