KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Tuesday, August 10, 2010

Mahabusu akutwa na silaha

KATIKA watuhumiwa 11,waliokatwa kwa makosa mbalimbali ya kihalifu yupo mahabusu mmoja amekamtwa akiwa silaha aina ya SMG na bastola

Akitoa taarifa hiyo, Kamanda Kova alisema, mahabusu huyo ni Marwa Chacha, mkazi wa Kipunguni, ambaye anakabiliwa na mashitaka unyang’anyi wa kutumia silaha ambapo mashitaka yake yapo katika mahakama ya Wilaya ya Ilala.

Alisema mahabusu huyo ni jambazi mzoefu na kiongozi wa majambazi maeneo ya Kipunguni na anamiliki kikundi cha majambazi na alikamatwa na silaha hizo katika gereza la Ukonga.

Kova alisema baada ya askari kumshtukia walimfatilia na kugundua anamiliki silaha hizo ndani ya agereza hilo.

Alisema mbali na kukamatwa na silaha hizo pia aliweza kukutwa na mashoka mawili na panga moja.

Kova alisema upelelezi zaidi unaendela na mtuhumiwaq huyo a tafikishwa tena wka mara ya pili kufunguliwa mashitaka ya kumiliki silaha hizo kinyume na sheria

No comments:

Post a Comment