KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, August 13, 2010

BP yakubali kulipa faini

Kampuni ya mafuta ya BP imekubali kulipa faini kwa kushindwa kuboresha viwango vya usalama katika mabomba ya mafuta ya Texas ambako watu kumi na watano walifariki dunia, kufuatia mlipuko kwenye mtambo wake mwaka 2005.

Idara ya usalama ya Marekani imesema BP italipa faini ya zaidi ya dola milioni hamsini,ikiwa ni kiwango kikubwa cha faini kuwahi kuamuriwa na idara hiyo.

Aidha imeafikiwa kuwa dola milioni mia tano zitumiwe kuboresha usalama katika mtambo huo.

Faini hiyo imetolewa kwa kuzingatia mabilioni ya dola ambazo BP ilikubali kulipa kwa hasara iliyosababishwa na kuvuja kwa mtambo wake wa mafuta kwenye ghuba ya Mexco.

No comments:

Post a Comment