KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, August 10, 2010

Akamatwa kwa kujif anya askari polisi

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limemkamata Daudi Ramadhani (24) kwa kukutwa amevaa sare za askari polisi alizoziiba mkoani Kigoma.


Kamanda wa Polisi Kanda Maalum , Suleiman Kova, aliwaambia waandishi kuwa , mtuhumiwa huyo alikamatwa maeneo ya Mvuti Msongola nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam akijifanya askari polisi.

Kova alisema, askari bandia huyo alikamatwa na askari wa doria waliokuwa maeneo hayo na alipotakiwa kujieleza alijitambulisha kuwa Konstebo Daudi wa namba G.4541 wa Ghala Kuu Dar es Salaam.

Alisema wakati wa kutakiwa kujieleza zaidi na kibano cha askari hao mtuhumiwa huyo alikiri kuwa yeye si askari na kukiri kuiba sare hizo mkoani Kigoma kwa askari aliyemtaja kwa jina la Edward.

Pia katika kukiri kwake aliwaeleza askari hao kuwa sare hizo alishazitumia katika matukio tofauti ya unyang’anyi na utapeli katika maeneo hayo ya Chanika na baa moja maarufu iitwayo Moshi Baa.

Kova alisema mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani muda wowote kujibu mashitaka hayo yanayomkabili.

No comments:

Post a Comment