KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, July 7, 2010

Zaidi ya watu 181 wapoteza maisha kwa pikipiki

IMEBAINIKA kuwa watu wapatao zaidi ya 181 wamefariki dunia kutokana na ajali zinazosababishwa na pikipiki ka kipindi cha miezi mitatu kuanzia Januari hadi Aprili mwaka huu.
Hayo yalibainika jana, na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama, Abbas Kandoro, alipobainisha hayo.
Alisema kuwa vifo hivyo vimesababishwa na ajali za pikipiki katika sehemu mbalimbali nchini na kubainisha kuwa jumla ya ajali hizo zimefikia 1,414 na kusababisha majeruhi wapatao 1,206.
Alisema baraza hilo limeamua katika kupunguza ajali hizo litahakikisha kila mwenesha pikipiki na abiria wanavaa kofia ngumu ili kupunguza majeruhi na vifo ambavyo havina ulazima.

Vifo hivyo vya pikipiki vimekuwa vikiongezeka siku hadi siku na usafiri huo kupanda chati kila kona ya jiji na mikoani.



Kufuatia ajali hizo zinazotokana na pikipiki kila kukicha hospitali ya taifa Muhimbli imetenga wodi maalum kuhusiana na matukio hayo ya pikipiki huku wengi wakiita ‘wodi ya pikipiki’.

No comments:

Post a Comment