KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Sunday, July 11, 2010

Washukiwa wa ugaidi wahukumiwa Tunisia

Wanaume wanane wamehukumiwa kwenda jela kwa vipindi hadi miaka 12 nchini Tunisia baada ya kupatikana na hatia ya kuchochea ugaidi, kulingana na wakili wao.

Wanaume hao walipatikana na hatia kwa makosa ya kuwa wanachama wa kundi la kiislam linalotetea vitendo vya kigaidi, wakili Sam Ben Amor, alisema. .

Wote walikana makosa hayo, na wakili wao hakutaja jina la kundi ambalo wanaume hao walihusishwa nalo.

Mahakama ya Tunisia ilitoa hukumu hiyo siku ya Jumamosi.

Wakili Ben Amor alisema: "vijana watatu walihukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 12 na wengine watano walihukumiwa vipindi vya miaka miwili hadi mitano.

"wawili kati yao walihukumiwa wakiwa nje ya nchi kwa vile walitorokea Ufaransa na Sweden ambako waliomba hifadhi ya kisiasa."



Wengine walidai kuwa waliteswa ili kukiri makosa, kama ilivyorepotiwa na shirika la habari la Associated Press.


Tunisia, mshirika wa karibu wa Marekani, imekuwa ikipambana na uasi wa wanamgambo wa kiislam katika miaka ya hivi karibuni ambapo iliwafunga jela watu takriban 1,000 waliotuhumiwa kupanga kupigana na wanajeshi wa kigeni wanao-ongozwa na Marekani nchini Iraq.

Shirika la Human Rights Watch limesema takriban wote waliohukumiwa chini ya sheria hizo walishtumiwa kupanga kujiunga na makundi ya wanamgambo nje ya nchi au kuwahimiza watu wengine kufanya hivyo, badala ya wao wenyewe kupanga au kufanya vitendo hivyo.

No comments:

Post a Comment