KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, July 17, 2010

Wakimbizi 2000 warejeshwa Rwanda

Wakimbizi wa Rwanda waliorejea nchini mwao kutoka kambi za Uganda wanasema kuwa walidhulumiwa kwa kurejeshwa kwa lazima. Wanasema kuwa polisi nchini Uganda waliwakamata kwa nguvu na kuwasafirisha kwa malori huku wakiwapiga risasi wale waliojaribu kutoroka.
Watu wawili walijeruhiwa walipojaribu kuruka kutoka malori yao. Zaidi ya wakimbizi 2000 wamerejeshwa nchini Rwanda kutoka Mbarara magharibi mwa Uganda.
Serikali ya Uganda imesema kuwa watu hao hawakuwa wakimbizi halali bali walikuwa

wanatafuta hifadhi katika mazingira bora kiuchumi, na kuwa waliagizwa waondoke Uganda kufikia mwanzo wa mwezi huu.

No comments:

Post a Comment