KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, July 14, 2010

Vijana Afrika 'wabadili tabia za ngono'


Mwathirika wa Ukimwi barani Afrika

Takwimu mpya zilizotolewa na Umoja wa Mataifa zimeonyesha kuenea kwa virusi vya HIV miongoni mwa vijana kwenye nchi zilizoathirika zaidi na ukimwi, hasa barani Afrika zimepungua.

Katika ripoti hiyo, UNAids imesema idadi ya watu wenye virusi vya HIV imepungua hadi kufikia asilimia 25 kutokana na vijana kati ya miaka 15-24 kubadili tabia zao za kujamiiana.

Ripoti hiyo imesema matokeo hayo ni kutokana na kampeni za kuzuia kuenea kwa virusi vya ukimwi.

Lakini Umoja wa Mataifa umesema umeongezeka Uganda, nchi iliyosifiwa kwa kupambana na ugonjwa huo.

Kulingana na umoja huo, vijana milioni tano wanaishi na virusi vya ukimwi duniani, na hivyo kuwepo na maambukizi mapya kwa asilimia 40.
' Onyo'

Kampeni kali ya Uganda dhidi ya HIV/Aids ilisaidia kupunguza kasi ya kuenea kwa virusi vya ukimwi -iliyofikia aslimia 30 katika miaka ya 1990.

Mkurugenzi mkuu wa UNAids Michel Sidibe ameiambia BBC, " Baada ya maambukizi hayo kupungua na kutolewa kwa matibabu, wengi wao hawakuwa na wasiwasi tena kama ilivyo mwanzo katika mipango ya kuzuia."

"Kwahiyo matokeo tunayoyashuhudia leo Uganda ni jambo linalotakiwa kututisha-hasa maendeleo yake na namna ya kuhakikisha idadi haiongezeki ambayo huenda kuridhika ndio kumesababisha hilo."

Alisema, hata hivyo takwimu nyingine ni ishara nzuri ya mabadiliko kwani vijana barani Afrika wamekuwa makini zaidi na afya zao.

" Kwangu mimi, hiyo ni hatua kubwa sana katika mipango yetu ya kuzuia."

No comments:

Post a Comment