KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Tuesday, July 20, 2010

Ubishi Wasababisha Alazwe Hospitali


Mwanaume mmoja nchini India amenusurika kufariki baada ya kummeza nyoka mwenye sumu kali baada ya wenzake kumbishia hawezi kufanya hivyo.
Mwanaume huyo aliyetajwa kwa jina la Zaver Rathod mwenye umri wa miaka 35 alimuua kwa mawe nyoka aliyemgonga rafiki yake katika mji wa Surat katika jimbo la Gujurat, limeripoti gazeti la The Times of India.

Zaver aliwatambia wenzake kuwa anaweza kummeza nyoka huyo mwenye sumu kali ambaye hakutajwa jina lake.

Kufuatia ubishi uliozuka, Zaver alidiriki kuyaweka maisha yake hatarini kwa kukubali kummeza nyoka huyo kwa dau dogo la rupia 100 ambazo ni sawa ni sawa na Tsh. 2500.

Zaver aliugua ghafla baada ya kummeza nyoka huyo kama alivyokuwa. Aliwahishwa hospitali akiharisha na kutapika sana.

Madaktari walifanikiwa kumtoa nyoka huyo toka tumboni mwake kabla sumu yake haijaingia kwenye mfumo wa damu ambapo maisha yake yangekuwa hatarini.

Zaver alitoroka hospitali leo akiwakimbia waandishi wa habari wa India ambao walifika hospitali kumhoji.

Madaktari wanatarajia Zaver atapona kabisa hali aliyo nayo sasa

No comments:

Post a Comment