KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Sunday, July 18, 2010

TLP yapata mgombea urais mpya


MKUTANO Mkuu wa Chama Cha Siasa, Tanzania Labour Party[ TLP] jana kilifanikiwa kumpitisha Mutamwega Mugahywa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao.
Mkutano huo uliowakutanisha wananchama wa chama hicho uliofanyika jijini Dar es Salaam na jumla ya wanachama wawili walikuwa wakigombania nafasi hiyo.

Katika kinyang’anyiro hicho alikuwa akigombania Muamwega Mugahywa na Maxmilian Lyimo ambapo, Mugahywa aliibuka kidedea na kupata kura 73 sawa na asilimia 91.76 na Lyimo kuambulia kura 11 sawa na asilimi 9.24 kati ya kura 84 zilizopigwa.

Mara baada ya uchaguzi huo kumalizika mgombea huyo aliwashukuru wapiga kura kwa kumchagua na kupa heshima hiyo na kuahidi kupeperusha bendera ya chama hicho vyema bila kuwangusha wanachama na kulta mapinduzi ndani ya chama hicho.

Alisema anatarajia kufanya kampeni zake kwa kutumia helikopta atakapokuwa akitembelea wapiga kura wake mikoani na anatarajia kuwa rais wa nchi hii na akiwa madarakani anatarajia kuchagua waziri mkuu mwanamke kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii.

No comments:

Post a Comment