KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Sunday, July 18, 2010

Mwanamke mwizi wa magari akamatwa


JESHI la polisi nchini, linamshikilia mwanamke [jina kapuni] mwizi wa magari baada ya kukutwa akiwa na magari matano ya wizi.

Taarifa hiyo ilitolewa jana na Kaimu Kamanda wa Kanda maalumu ya Dar es Salaam, Charles Kenyela, kuwa mwanamke huyo alikamatwa na magari hayo matano na mawili kati yao ni aina ya Toyota Land Cruizer Pick Up na lingine Toyota Mark II mali ya shirika la umeme nchini (Tanesco).

Kenyela alisema gari la Tanesco hilo lilibainika na liliibiwa Julai 11, mwaka huu majira ya saa 7 usiku, huko maeneo ya Mikocheni kwenye ofisi ya Tanesco wilaya ya Kinondoni.

Kenyela alisema mwanamke huyo alikutwa na dereva mmoja wakiwa katika harakati za kubandika gari hilo namba za bandia na katika upelelezi zaidi waligundua kuna magari mengine zaidi mahali hapo.

Hivyo mwanamke huyo anashikliwa na polisi kwa upepelezi wa kina na alubainika alikuwa akiiba magari hayo kwa kutumia funguo bandia.

No comments:

Post a Comment