KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Sunday, July 18, 2010

Mwanamke akamatwa kwa kuiba kanga za msikitiniMWANAMKE mmoja ambaye haikufahamika mara moja ni mkazi wa wapi, alipata aibu kubwa baada ya kushindwa kufanikiwa kuiba kanga zinazotengwa maalum kwa ajili ya kusalia na kukutwa akitoka na mfuko aliohifadhia kanga hizo msikitini humo.
Mwanamke huyo hakufanikiwa kufanya ufirauni huo, Ijumaa ya wiki iliyopita katika msikiti mmoja wa Ijumaa wa maeneo ya Mabibo Mwisho.

Mwanamke huyo alitinga msikitni hapo mapema kwa kujifanya ana lengo la kusali Sala ya Ijumaa na kumbe alikuwa na dhamira nyingine nje ya hiyo, wakati anaingia hakumkuta mtu ndani ya msikiti huo na alitumia muda huo kujichagulia kanga azipendazo zipatazo doti nne [peace nane ] na alizihifadhi kwenye mfuko ili aweze kuondoka nazo kwa matumizi binafsi ambayo hayakufahamika mara moja.

Mungu si athumani wakati anajitayarisha kutoka na kupepesa macho huko na huko kwenye majira ya saa sita kasoro hakuona mtu na alichukua mfuko wake kwa lengo la kuondoka nazo na kuacha swala hiyo bado haijasaliwa.

Ghafla wakati anafika mlango wa kutokea, mwanamke mwingine alikuwa naingia msikitini humo kwa lengo la kuja kusali Ijumaa na kukutana nae akiwa na mfuko huo na kumsalimia na aliitikia kwa wasiwasi na mwanamke huyo alipatwa na wasiwasi na kumuangalia mkononi alimuona amebeba mfuko huo.

Mwanamke huyo kwa kuwa alikuwa ni mzoefu na msikiti huo alikuwa na wasiwasi kwa kuwa matukio ya wizi huo wa kanga msikitini hapo yalikuwa yakifanyika bila mafanikio ya kumpata muhusika.

Hivyo alimuomba radhi mwanamke huyo asimame na kumuomba amuonyeshe kwenye mfuko huo alikuwa amehiadhi kitu gani, mwanamke mwizi alimjibu kuwa alikuwa amehifadhi vitu vyake na alipoulizwa kwa nini alikuwa akitoka msikitini muda huo hakuwa na jibu na kupatwa na aibu kubwa.

Wakati mazungumzo kati yao yakiendelea, wanawake wengine wawili walikuwa wakiingia msikitini humo na yule mmoja kuwataka wenzake hao wawili wampekue mwanamke huyo kwa kuwa yeye alikuwa na wasiwasi nae kwa kile alichokibeba kwenye mfuko huo.

Hawakuweza kuamini macho yao walipofungua mfuko huo walikutana na vipande vya kanga vilivyohifadhiwa msikitini humo kwa ajili ya wanawake wanaofika msikitini hapo kusalia.

Ndipo wanawake hao walipomtaka mwizi huyo arudi msikitini ili waumini wengine waongezeke aonyeshwe kuwa yeye ndiye mwizi anayeiba kanga msikitini humo na waumini wengine wapate kumtambua.

Aliwaomba radhi wamuachie lakini hawakumuachia na waumini wengine walizidi kuongezeka na kila mmoja alimuona na kupata aibu kubwa.
Mtandano huu nao ulibahatika kumuona mwanamke huyo na alipotakiwa kujieleza kanga hizo anakwenda kuuza ama kwa matumizi yake binafsi ya nyumbani hakuwa na majibu kutokana na aibu kubwa aliyogubikwa nayo usoni aliyoipata katika nyumba hiyo ya ibada na kisha mwanamke huyo kuachiwa aondoke zake na aliweza kutoka nje ya msikiti huo bila haya na kuacha wamumini wengine wakipata hotuba za hapa na pale.

Awali kwa mara ya kwanza mtandao huu, ulipofika msikiti hapo mwezi Aprili mwaka huu ulikuta wanawake walilalama hapa na pale kuwa kuna wizi wa kanga umetokea msikitini humo na kutangaza msikitini humo kuwa kama kuna muumini ana tabia ya kuondoka na kanga aache tabia kwa kuwa ilikuwa haimpendezi Mungu.

Kwa kuwa siku za mwizi ni arubaini mwanamke aliyekuwa akifannya vitendo hivyo na wengi walisema atakuwa ndiyo muhisika na wizi uliotokea siku za nyuma alikamatwa msikitini hapo

No comments:

Post a Comment