KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Sunday, July 18, 2010

Mwanachama CCM aichangia Chadema Sh. Milion 100


MFANYABIASHARA maarufu nchini mwenye asili ya kiasia, Mustapha Jaffar Sabodo, mabaye pia ni mwanachama mzuri wa Chama cha Mapinduzi (CCM) amekichangia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kiasi cha shilingi milioni 100 ka kuvutiwa na chama hic
Sabodo alikabidhi hundi ya mchango huo nyumbani kwake jana, Upanga jijini Dar es Salaam, kwa viongozi wakuu wa chama hicho akiwemo Mwenyekiti Taifa, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk.Wilbrod Slaa akiwemo Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa chama hicho, Antony Komu.

Mara baada ya kukabidhi hundi hiyo Sabodo alisema, licha ya kuwa yeye ni mwanachama CCM kwa miaka mingi amevutiwa na jinsi chama hicho kinavyoendesha siasa nchini kwa kuwa viongozi wake ni makini na wana uchungu na maendeleo ya nchi hii

Pia alisema lengo ya kutoa mchango huo ni kuleta usawa katika demokrasia nchini katika uendeshaji wa shughuli za kisiasa na kuona demokrasia inakua na upinzani unaimarika.

“Nitaendelea kuwa mwanachama halali wa CCM, na kufanya kwangu hivi ni kuitaka CCM isilale isibweteke” alisema Sabodo

Kwa upande wa viongozi hao walimshukuru sana mfanyabiashara huyo kwa kuonyesha kutaka demokrasia ya kweli ndani ya nchi hii kwa kutoa kiwango kikubwa cha fedha tena hadharani kuichangia Chadema kinyume na matarajio yao.

Walisema fedha hizo watazitumia kama ipasavyo katika vipaumbele vitakavyopangwa na kamati kuu na kuendeleza mipango endelevu na kuimarisha zaidi chama hicho na kujiandaa na uchaguzi tarajio wa Oktoba mwaka huu.

No comments:

Post a Comment