KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, July 7, 2010

MTOTO wa miaka 10 aliyekuwa akisoma darasa la pili, amefariki dunia baada ya kubakwa


MTOTO wa miaka 10 aliyekuwa akisoma darasa la pili, amefariki dunia baada ya kubakwa na mtu zaidi ya mmoja wasiofahamika huko kitongoji cha Bangwe, Sumbawanga.

Taarifa ya polisi iliyothibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, Bw. Isuto Mantage ilisema kuwa, tukio hilo lilitokea juzi kasha mwili huo kutelekezwa.


Kamanda Mantage alisema kuwa, kutokana na maelezo ya mama wa mtoto huyo yalisema, siku ya tukio mtoto huyo alimuaga mama yake kuwa anakwenda kumsalimia dada.

Alisema ilipofika jioni motto huyo hakurudi na mama yake huyo alijua aliamua kulala kwa dada yake jambo ambalo alihisi kwa kuwa mara nyingine huamua kulala huko kumbe haikuwa hivyo.
.
Alisema baada ya kufanfya mawasiliano na kubaini kuwa motto huyo hayupo kwa dada yake huyo alitoa taarifa kwenye vyombo husika na katika msako waliukuta mwili huo ukiwa katika jumba ambalo hawaishi watu na mdomo wake ukiwa amezibwa kwa kujazwa matambara.

Alisema kabla mwili huo haujachukuliwa mahali hapo walifanya vipimo vya daktari na kubaini kuwa mwili huo ulibakwa kwa zamu na kusababisha kifo hicho.

Mwili huo ulichukuliwa na kwenda kuhifadhiwa huku wauaji wamtoto huyo wakisakwa kwa udi na uvumba kwa nguvu ya kushirikiana kati wa wananchi na jeshi la polisi mkoani humo.

No comments:

Post a Comment