KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Sunday, July 18, 2010

Mporogomyi afata nyayo za Chenge


MBUNGE wa Kasulu Magharibi CCM, Kilontsi Mporogomyi amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mkoa wa Dodoma kwa kosa la kugonga na kuua mtembea kwa miguuu.
Mbunge huyo alifikishwa mahakamani hapo jana, na kusomewa mashitaka na Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Beatrice Nsana, mbele ya Hakimu Mkazi Hassan Momba wa mahakama hiyo.

Nsana alidai kuwa, mtuhumiwa alitenda kosa hilo Julai 11, mwaka huu, majira ya saa 5.30 usiku, huko eneo la Wajenzi, mjini Dodoma.

Alidai kuwa, mtuhumiwa akiwa akiendesha gari namba T288ASJ aina ya Toyota Land Cruiser akashindwa kusimama na kumpisha mtembea kwa miguu kwa wakati huo avuke barabara na hatimaye akamgonga na kusababisha kifo papohapo.

Hata hivyo ilidaiwa kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika, na mshitakiwa kukana mashitaka hayo mawili ya kuendesha gari kizembe na kusababisha kifo cha mtu mmoja.

Hata hivyo mtuhumiwa huyo aliweza kuachiwa huru kwa kupata dhamana ya kutakiwa kuwasilisha Shilingi milioni 5, kesi hiyo pia iliahirishwa na itarudi tena mahakamani hapo Agosti 5 mwaka huu kwa kutajwa.

No comments:

Post a Comment