KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, July 10, 2010

Matizo ya moyo huenda yalisababisha kifo cha Chebeya

Kundi la wachunguzi wa kimatibabu wa kimataifa wanaochunguza chanzo cha kifo cha mwanaharakati wa kutetea haki za kibinadam nchini jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wamesema hawajafanikiwa kutambua kile kilichosababisha kifo hicho.

Wachunguzi hao wanasema kifo hicho huenda kilisababisha na matatizo ya moyo.

Mwili wa Floribert Chebeya, ulipatikana ndani ya gari lake huku mikono yake ikiwa imefungwa, siku moja tu baada ya kuamriwa kufika mbele ya afisa mkuu wa polisi nchini humo, John Numbi.

Chabeya alifahamika kutokana na juhudi zake za kupinga mauaji ya kiholela nchini Congo.

Kifo chake kilisababisha raia wa nchi hiyo na wanaharakati wa kuetetea haki za kibinadamn kuitisha uchunguzi wa kimataifa.

Ilifahamika wazi kuwa Bw. Chabeya alikuwa na matatizo ya moyo kwa muda mrefu.

Madaktari kutoka Uholansi kwa ushirikiano na wenzao kutoka Congo walifanya uchunguzi huo.

No comments:

Post a Comment