KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Tuesday, July 20, 2010
Kila Siku Mwanajeshi Mmoja wa Marekani Anajiua Afghanistan
Idadi ya wanajeshi wa Marekani waliopo nchini Afghanistan na Iraq ambao wanajiua kutokana na stress za vita inaongezeka kwa kasi ikiashiria kuwa kila siku mwanajeshi mmoja wa Marekani anajiua.
Kwa mujibu wa takwimu za jeshi la Marekani idadi ya wanajeshi wa Marekani wanaokatisha maisha yao wao wenyewe imeongezeka kwa kasi pamoja na kwamba jeshi la Marekani linajitahidi kuwapa tiba ya stress wanajeshi wake.
Mwezi juni pekee kulikuwa na jumla ya wanajeshi 32 waliojiua wenyewe kutokana na stress mbalimbali za vita.
Mwaka jana kulikuwa na jumla ya wanajeshi wa Marekani 244 ambao walijiua wenyewe nchini Iraq au Afghanistan.
Jeshi la Marekani lilikuwa likitarajia kupungua kwa idadi ya wanaojiua mwaka huu kulinganisha na mwaka jana kutokana na programu mbalimbali walizozianzisha za kuwasaidia wanajeshi wanaosumbuliwa na stress za vita.
"Tunasikitishwa sana na idadi kubwa ya wanajeshi waliojiua mwezi juni kwasababu tunaamini kwamba programu na taratibu za ushauri tulizoziandaa zinawasaidia wanajeshi wenye matatizo", alisema kanali Christopher Philbrick ambaye ni mkurugenzi wa idara ya kuzuia wanajeshi wa Marekani kujiua
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment