KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, July 7, 2010

Kichanga chatupwa njiani kikiwa hai

SIJUI ni kutokana na maisha magumu yaliyopita kiasi mkoani Dar es Saalaam, ama ni ukatili wa mtu binafsi hali kila kukicha matukio ya utupaji vichanga hayapungui.
Leo asubuhi majira ya saa 12 asubuhi, wakazi wa eneo la Ulongoni “A’ walishuhudia kichanga kikiwa kimezungushwa kanga mbili na kutupwa barabarani huku kikiwa hai hali iliyofanya kushangazwa na tukio hilo.

Imedaiwa kuwa kichanga hicho cha kike, kinachokadiriwa kuwa na umri usiozidi wiki moja alitupwa katika moja ya njia ya maeneo hayo.

Ilidaiwa kuwa watu walipokuwa wakilaumu kwa masikitiko kuhusiana na tukio hilo huku wakimlaumu mwanamke aliyetupa kichanga hicho watu wawili waliwataka wakazi hao kutolaumu sana kwa kuwa walihisi huenda akawa aliyetupa kichanga hicho ni mpungufu wa akili aliyekuwa akionekana amepinga kambi maeneo hayo.

Walidai siku tatu nyumba wakati wanapita njia hiyo walimuona mwanamke kichaa akiwa mjamzito na walidai huenda akawa kichaa huyo alijifungua na kutupa kichanga hicho.

HAta hivyo baadhi ya watuw alipoamua kuzunguka kuanalia huenda watamuona kichaa huyo hawakumuona mahali.

No comments:

Post a Comment