KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, July 17, 2010

Jundullah wawaua zaidi ya watu 20 - Iran


Maafisa nchini Iran wanasema kuwa zaidi ya watu 20 wameuawa na wengine 100 kujeruhiwa katika shambulio la kujitoa mhanga nje ya msikiti mmoja wa kishia kusini mwa mji wa Zahedan.
Naibu wa waziri wa usalama wa ndani Ali Abdollahi amesema kuwa mlipuko wa kwanza ulitokea katika kituo kinacholindwa na maafisa wa chama cha mageuzi. Shambulio hilo limetokea siku chama hicho kinaadhimisha kuundwa kwake.


Kundi la dhehebu la sunni Jundullah limedai kuhusika na shambulio hilo. Iran ilimhukumu kifo kiongozi wa kundi hilo Abdul Malik Rigi mwezi uliopita. Serikali ya Iran imekuwa ikishutumu Marekani na Pakistan kuwa inaunga mkono kundi hilo la Jundullah.

No comments:

Post a Comment