KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, July 7, 2010

Hispania yaidizi nguvu Paraguay 1-0

David Villa alifunga goli lake la tano katika fainali za Kombe la Dunia 2010 kuipatia Hispania goli pekee na nafasi ya kucheza nusu fainali na kuitoa Paraguay katika mechi iliyokuwa na ukame wa muda mrefu.

Goli hilo la dakika 82 lilipatikana baada ya kugonga mwamba, kabla ya kurudi kutikisa nyavu, Villa akimalizia mpira wa Pedro aliyeingia kipindi cha pili.

Ilikuwa mechi ngumu kwa Paraguay ambao walikosa penati iliyopigwa na Oscar Cardozo na mlinda mlango Iker Casillas kuicheza.

Hiyo ilikuwa ni katika dakika ya 57 - na kabla ya muda kupita, Hispania walizawadiwa penati na mwamuzi Carlos Batres.

Katika hali iliyotegemewa, Xabi Alonso alitikisa nyavu, lakini akaambiwa apige tena mkwaju wa penati kwasababu wachezaji wa Hispania walitoka mapema kucheza, ya pili ikaokolewa.

This content requires Flash Player version 10 (installed version: No Flash Flayer installed, or version is pre 6.0.0

No comments:

Post a Comment