KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, July 19, 2010

Dawa za Kulevya TZ - Vijana waathirika

Dawa za kulevya ni kosa la jinai katika nchi nyingi duniani. Lakini matumizi ya dawa hizo, hususan miongoni mwa vijana nchini Tanzania, umekita mizizi kwa sababu dawa za kulevya kama vile bangi hupatikana kwa urahisi nchini humo.

Ngwandume Joseph, alielezea BBC kuwa alianza kuvuta bangi tangu utotoni, tabia iliyomuingiza mashakani.


" Mimi nilianza kuvuta bangi nikiwa darasa la sita. Nilijiunga na vijana waliokuja shuleni kucheza mpira na nikadhani kuwa ni ujasiri kujiingiza katika matumizi hayo". Asema Ngwandume. Lakini aligundua kuwa sio sifa bali anajijutia." kutokana na tabia mbaya niliyoshika, nilifukuzwa shule licha ya kuwa nilikuwa nimefuzu vizuri. Sasa najuta"
Serikali inasemaje?

Tume inayodhibiti dawa za kulevya inakiri kwamba mtandao wa wafanyibiashara vigogo unachangia kurudisha nyuma vita dhidi ya dawa za kulevya. Kamishna mkuu wa tume hiyo nchini Tanznia ni Christopher Shakiondo. " Bangi kwa mfano inalimwa katika sehemu nyingi na inapatikana kwa urahisi sana. Wengine wanalima hata nyuma ya nyumba zao na hivyo watoto pia wanaweza kupata".

Sasa vijana walioathirika na dawa kama hizo wamepiga moyo konde na kuamua kuanza maisha upya kwa matumaini.

Ngwandume alieleza BBC siri yake." Tulipata elimu muhimu shuleni kuwa tuangalie 3Ts. Tatizo - Tatuzi na Tokeo. Ukifikiria hizi basi utajua ni wapi unelekea au ni nini kitakachotokea hapo mbeleni - na utaweza kujiamulia hatma yako".

No comments:

Post a Comment