KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, July 10, 2010

Chama cha CCM kuteua wagombea wa urais


Wajumbe wa chama tawala nchini Tanzania, Chama cha Mapinduzi, CCM, wanakutana leo mjini Dodoma, kuwateua wagombea wa Urais wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania pamoja na wagombea wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.

Kumekuwa na kampeini za usiku kucha huku wagombea wakiwashawishi wajumbe kuwaunga mkono.
Rais Jakaya Kikwete

Rais Jakaya Kikwete

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari nchini humo, watu watano wamejitokeza kuwania kiti cha Urais kisiwani Zanzibar.

Watano hao ni pamoja na waziri wa zamani Dr Mohamed Bilal, makamu wa rais Dr Ali Mohamed Shein, waziri kiongozi Shamsi Vuai Nahodha, na naibu wake Ali Juma Shamhuna na waziri wa elimu Amali Haroun Ali Suleiman.

Watano hao watakuwa wakiwania nafasi ya kumrithi rais Amani Karume ambaye muda wake wa kuhudumu kama rais unamalizika mwaka huu.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano Jakaya Kikwete, anatarajiwa kuidhinishwa tena kuwania kiti hicho kwa muhula wa pili.

Kufikia sasa hakuna mwanasiasa yeyote ambaye amejitokeza kumpinga rais Kikwete. Matokeo ya kongamano hilo yanatarajiwa kutolewa baadaye hii leo.

No comments:

Post a Comment