KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Sunday, July 18, 2010

Awa kero kwenye nyumba ya kupanga


KIJANA aliyetambulika kwa jina moja la Said [30] mkazi wa Tandika Maguruwe, amejikuta akichukiwa na wapangaji wenzake kwenye nyumba anayoishi kwa kuwa na tabia chafu ya kuwakutanisha wanawake mara kwa mara na kusababisha ugomvi unaowakera wengine
Kijana huyo ambaye imefikia kila mpangaji katika nyumba hiyo [namba kapuni] kumchukia kwa tabia yake hiyo ya kusababisha ugomvi mara kwa mara na kuvunja amani kwa wapangaji wenzie.

Kufuatia hali hiyo ya kukerwa na walio wengi imefikia wapangaji wawili waishio humo kumsaka mwandishi wa nifahamishe arushe kero hiyo huenda itakuwa fundisho kwa kijana huyo.

Watu hao walidai kuwa nyumba yao ni ina jumla ya vyumba kumi na mmiliki wa nyumba hiyo haishi hapo na ndio chanzo cha vituko katika nyumba hiyo ambapo kila mmoja anajichukulia maamuzi yake.

Walidai kuwa kijana huyo amekuwa na tabia chafu ya kukutanisha wanawake chumbani kwake ama wamekuwa wakifumaniana na wamekuwa waksababisha vurugu kubwa kwenye nyumba hiyo na akiona mambo yameharibika huwa anatoweka na kuwaachia varangati wapangaji wengine kuwagombelezea wanawake hao.

Hali hiyo wamedai wameshaishuhudia zaidi ya mara mbili na kuonywa lakini haikuleta mafanikio kwa kijana huyo.


Walidai wasichana wanapokutana na kujijua wote ni wapenzi wa kijana huyo huwa hapatoshi kwa muda huo, kubwa ya yote ugomvi wa mara ya tatu uliotokea jumapili ya wiki iliyopita ulikuwa ni funga mwaka baada ya mchumba wake kumfumania akiwa na msichana mwingine wakijivinjari ndani ya chumba hicho.

Ilidaiwa kuwa msichana aliyefahamika kwa jina la Feti ambaye wengi ndani humo wanamtambua kama mchumba halali wa kijana huyo alifika nyumbani kwa mchumaba wake huyo bila taarifa majira ya saa mbili usiku, baada ya kutonywa na wasamaria wema kuwa mchumba wake ameonekana kuingiza msichana kwenye chumba chake.

Bila matarajio ya Saidi, Feti alitinga hapo na kubaki amishangaa kwa kuwa siku mbili nyuma alimuaga anakwenda mkoani Tanga kusalimia wazazi wake na kushangazwa na hali hiyo.


Ilidaiwa kuwa, Feti alipofika hapo na kubisha hodi Said hakuwa na mashaka ya kufungua kwa kujua mchumba wake huyo hakuwemo jijini na hakuamini alichokiona machoni mwake na Feti kuingia moja kwa moja chumbani kwake na kumkuta msichana mwingine akiwa ametuli kwenye sofa bila ya wasiwasi.

Ilidaiwa kuwa kipigo cha nguvu kilianza kwa msichana huyo, na alipozidiwa Sidi alijaribu kumgombelezea nae alionekana kushindwa kwa kuwa Feti alikuwa amejiandaa kwa tukio hilo na hatimaye msichana huyo nae alifanikiwa kujinasua kwenye kipigo hicho na kuanza vurumai za aina yake hali iliyosababisha kuvunjika kwa amani ndani ya nyumba hiyo.

Ilidaiwa kuwa msichana huyo alianza kurusha vitu mbalimbali zikiwemo chupa na mawe hata hivyo watu walimsihi aondoke mahali hapo na alionekana kua mbishi na kuendelea kurusha mawe na kusababisha motto wa mpangaji mmoja kujeruhiwa na jiwe hilo na kipigo kumrudia tena kwa mara nyingine.

Wakati yote hayo yanaendelea ilidaiwa kuwa Saidi alishaondoka mahali hapo hali hiyo ndiyo ilionekana kuakera watu zaidi kukimbia majukumu ambayo ameyatengeneza mwenyewe na kuwaachia raia wengine kujiingiza katika majukumu ambayo hayakuwa yao.

Hata hivyo kwa mujibu wa maelezo ya wapangaji hao walidai kuwa wana mkakati wa kumpelekea tarifa mwenye nyumba wao anayeishi mkoani Mtwara ili Said aweze kumuhamisha ili waweze kubaki kwa amani kwa kuchoshwa na tabia zake.

No comments:

Post a Comment